Tuesday, June 11, 2019
Mwenge yarudi Ligi kuu Zanzibar
Klabu ya Mwenge imerudi tena Ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao baada ya kukabaliwa rufaa yake na kamati ya rufaa na usuluhisho baada ya ZFA wakati huo kushindwa kutekeleza kanuni yake ya mashindano na kuishusha klabu hiyo kinyume na utaratibu wa kikanuni 2018/2019.
Kwa mujibu wa barua iliotelewa na kamati ya rufaa kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar yenye namba ya kumbu kumbu ZFF/NV/96/VOL41/262 2019 imesema kamati ya rufaa na usulihisho imeirejesha klabu ya Mwenge kwenye Ligi kuu ya Zanzibar baada ya kusikiliza maombi ya klabu hiyo.
Katika maelezo ya klabu ya Mwenge imelalamiki kamati ya rufaa na usulihishi kuwa ZFA wakati huo ilishindwa kutaja kifungu cha kanuni kilichoishusha klabu hiyo daraja la kwanza, ZFA wakati huo ilishindwa kusimamia kanuni ya mashindano inayosema Ligi itachezwa na vilabu 20 badala yake Ligi kuu Zanzibar imechezwa na vilabu 19 bila ya muongozo wa ZFA.
Kwa upande wake Kamati ya rufaa na Usulihishi chini ya Mwenyekiti wake Taki Abdulla Habibu wamekubali ombi la rufaa la klabu ya Mwenge na kutupulia mbali uamuzi uliotolewa na ZFA kupitia kamati ya maridhiano sasa klabu hiyo itacheza tena Ligi kuu ya Zanzibar msimu huu 2019/2020.
Katika hatua nyengine kamati ya rufaa imekubali ombi hilo baada ya kujiridhisha kuwa ZFA wakati huo ilishindwa kutekeleza kanuni ya kifungu cha 4 (1) kuwa Ligi kuu ya Zanzibar itachezwa na vilabu 20 na vilabu 6 na Ligi kucheza kuchezwa na vilabu 19.
Kwa upande mwengine kamati kupitia barua yake imegundua ZFA wakati huo ilishindwa kuandikia barua klabu ya Shaba kuwa imeshuka daraja wakati imeshindwa kucheza Ligi kuu ya Zanzibar na kanuni shaba inatakiwa kushushwa madaraja mawili kwa kushindwa kucheza Ligi kuu ya Zanzibar na kupelekea Ligi hiyo kuchezwa na timu 19 sio 20.
Mwisho barua hiyo imeamua rasmi na kutoa muongozo kuwa klabu ya Mwenge itacheza Ligi kuu ya Zanzibar na Shaba itacheza Ligi Daraja la kwanza msimu huu 2019/2020.
Subscribe to:
Posts (Atom)