ZAN SPORT NEWS
Tuesday, June 11, 2019
Mwenge yarudi Ligi kuu Zanzibar
Klabu ya Mwenge imerudi tena Ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao baada ya kukabaliwa rufaa yake na kamati ya rufaa na usuluhisho baada ya ZFA wakati huo kushindwa kutekeleza kanuni yake ya mashindano na kuishusha klabu hiyo kinyume na utaratibu wa kikanuni 2018/2019.
Kwa mujibu wa barua iliotelewa na kamati ya rufaa kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar yenye namba ya kumbu kumbu ZFF/NV/96/VOL41/262 2019 imesema kamati ya rufaa na usulihisho imeirejesha klabu ya Mwenge kwenye Ligi kuu ya Zanzibar baada ya kusikiliza maombi ya klabu hiyo.
Katika maelezo ya klabu ya Mwenge imelalamiki kamati ya rufaa na usulihishi kuwa ZFA wakati huo ilishindwa kutaja kifungu cha kanuni kilichoishusha klabu hiyo daraja la kwanza, ZFA wakati huo ilishindwa kusimamia kanuni ya mashindano inayosema Ligi itachezwa na vilabu 20 badala yake Ligi kuu Zanzibar imechezwa na vilabu 19 bila ya muongozo wa ZFA.
Kwa upande wake Kamati ya rufaa na Usulihishi chini ya Mwenyekiti wake Taki Abdulla Habibu wamekubali ombi la rufaa la klabu ya Mwenge na kutupulia mbali uamuzi uliotolewa na ZFA kupitia kamati ya maridhiano sasa klabu hiyo itacheza tena Ligi kuu ya Zanzibar msimu huu 2019/2020.
Katika hatua nyengine kamati ya rufaa imekubali ombi hilo baada ya kujiridhisha kuwa ZFA wakati huo ilishindwa kutekeleza kanuni ya kifungu cha 4 (1) kuwa Ligi kuu ya Zanzibar itachezwa na vilabu 20 na vilabu 6 na Ligi kucheza kuchezwa na vilabu 19.
Kwa upande mwengine kamati kupitia barua yake imegundua ZFA wakati huo ilishindwa kuandikia barua klabu ya Shaba kuwa imeshuka daraja wakati imeshindwa kucheza Ligi kuu ya Zanzibar na kanuni shaba inatakiwa kushushwa madaraja mawili kwa kushindwa kucheza Ligi kuu ya Zanzibar na kupelekea Ligi hiyo kuchezwa na timu 19 sio 20.
Mwisho barua hiyo imeamua rasmi na kutoa muongozo kuwa klabu ya Mwenge itacheza Ligi kuu ya Zanzibar na Shaba itacheza Ligi Daraja la kwanza msimu huu 2019/2020.
Wednesday, January 30, 2019
ZFA kuja na mipango kazi
Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetangaza kuwa na mpango kazi wake wa maendeleo kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 kwa ngazi zote zinazo husu mpira Zanzibar.
Akizigumza na wandishi wa habari mkuregenzi wa ufundi wa ZFA Salum Ali Haji amesema ZFA baada ya muda mrefu kushindwa kufanya mipango yake ya uhakika sasa kamati imeamua kuja na mipango ya maendeleo ya soka ndani ya visiwa vya Zanzibar wakianza na elimu ya mpira kwa wadau ili kujua maana ya mchezo huo unaopendwa lakini wamekosa ufahamu wa mchezo huo.
Aidha amesema kwa mwaka huu 2019 wamejipanga kuhakikisha Vijana wengi maskulini wanashiriki mchezo wa mpira wa miguu kutokana na umri wao na madaraja yanavyotakiwa ili kuweza kutoa wachezaji wengi maskulini wenye uwezo wa kucheza mpira kwenye viwango vya kimataifa.
Kwa upande mwengine amesema mwaka 2019/2020 ZFA itakuwa na mikakati ya maendeleo ya kukuza soka kwa kutoa mafunzo kwa makocha wote wasio na leseni hata moja na wale wenye leseni ndogo kupatiwa mafunzo ya juu ya ukufunzi ili kwa mwaka huo Zanzibar kuwe na wakufuzi wenye leseni kubwa, Salum amesema mafunzo mengine ni ya Udaktari wa viungo na michezo na semina za uongozi wa mpira kwa viongozi wote kunzia Wilayani hadi ZFA Taifa.
‘’Tumekaa na Wizara ya Elimu kupitia idara ya Elimu na Michezo tumehakikisha tunafanya mashindano ya Vijana ya maskulini ya Wilaya na kundaa Vijana kuwa wakufunzi na waamuzi wa baadae jambo hili lilikuwepo ila sasa ZFA tunakwenda kulifufua’’ Alisema Salum Haji.
Stika ataka sera ya ya filamu itekelezwe
Chama cha wasanii Filamu Zanzibar wameiomba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuharikisha kupitishwa sera yao ya Filamu na maigizo ya mwaka 2015.
Akizugumza na Gazeti hili Katibu wa chama cha Filamu Zanzibar Salum Maulid Salum (Stika) amesema kwa muda mrefu baada ya kupitisha sera hiyo mwaka 2015 ya rasimu ya pili mpaka leo sera hiyo bado haijafanyiwa kazi na kufanya chama chao kutokuwa na sera ya kufanya kazi zao kitaalam.
Aidha Salum Stika amesema sera hiyo itapopitishwa kwenye Baraza la Wakilishi na kupatiwa michango chama chao kitakuwa na jitihada ya kuhakikisha filamu za maigizo Zanzibar zinakwenda kufanyiwa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na kuendeshwa katika viwango vikubwa.
Kuhusu Soko la Filamu Zanzibar amesema wasanii wengi Zanzibar wanalalamikia mfumo wa soko Zanzibar lakini amesema changamoto hiyo itandoka baada ya sera ya mwaka 2015 kufanyiwa marekibisho na Baraza la wakilishi.
‘’Tunamuomba sana Wazara ya Vijana Sanaa na Michezo ihakikishe mwaka huu sera yetu ya sanaa ya Filamu na Maigizo inapelekwa kwenye Baraza la wakilishi na kufanyiwa marekibisho ili kuwa katika viwango vya ubora’’ Alilimalizia Salum Stika.
Friday, January 25, 2019
Hi hapa ratiba ya Kombe la FA mzunguko wa mwanzo Zanzibar
ZANZIBAR FA CUP
RATIBA YA MASHINDANO KOMBE CHAMA CHA MPIRA ZANZIBAR
FA CUP -UNGUJA
2019
S/NO SIKU TAREHE TIMU ZINAZOSHINDANA KIWANJA MUDA
1 JUMAMOSI 2 Feb-19 BWELEO KILIMANI CITY MAUNGANI 10:00
2 MFENESINI KIJICHI MISUKA 10:00
3 DULLA BOYS MPAPA WHITE BIRD 10:00
4 MAHONDA KIDS KWEREKWE CITY WHITE BIRD 8:00
5 NEW KING NEGRO MISUKA 08:00
6 UJAMAA KIZIMKAZI MAUNGANI 08:00
7 WHITE BIRD SUPER TIGER BUNGI 08:00
8 CHARAWE MWEMBELADU BUNGI 10:00
9 GULIONI MCHANGANI UTD AMAAN 10:00
10 SEBLENI SHARP BOYS AMAAN 08:00
11 JUMAPILI 3 Feb-19 MCHANGANI STR KUNDEMBA MISUKA 10:00
12 RASKAZONE UHAMIAJI AMAAN 08:00
13 KIMBUNGA ZANTEX MAUNGANI 08:00
14 VILLA FC AFRICAN COAST MCHANGANI 10:00
15 POLISI BRIDGE TA/JANG`OMBE AMAAN 10:00
16 MUNDU KIJANJA MAUNGANI 10:00
17 IDUMU SHANGANI WHITE BIRD 08:00
18 NGOME MAUNGANI WHITE BIRD 10:00
19 BLACK MAMBA NEW BOYS BUNGI 08:00
20 WEMBE KITOPE BUNGI 10:00
NB:
1. KIKAO CHA MATAYARISHO YA MCHEZO (PRE MATCH MEETING) NI SIKU MOJA KABLA YA MECHI SAA NNE KAMILI OFISI YA ZFA TAIFA.
2. TIMU ZINATAKIWA KUFIKA KIWANJANI NA MIPIRA MIWILI INAYOFAA KUCHEZEA. NA IKABIDHIWE KWA KAMISHNA WA MCHEZO KABLA YA MCHEZO KUANZA.
3. KAMA ITATOKEA MECHI KUTOKA SARE BAADA YA DAKIKA 90 SHERIA YA PENALTI ITATUMIKA.
“fair play”
BMTZ vyama vinaweza kujiendesha zanzibar
Baraza la Michezo Zanzibar (BMTZ) limejipanga kuhakikisha vyama vya michezo Zanzibar vinaweza kujiendesha bila ya kutegemea ruzuku ya Baraza la Michezo inayotolewa kwa kila chama cha Michezo .
Akizugumza na Mtandao huu Katibu Mtendaji wa BMTZ Zanzibar Khamis Abdalla Mzee amesema kwa mwaka 2019 BMTZ imefanyia marekibisho sera ya michezo Zanzibar ili kuona sekta ya michezo Zanzibar inapiga hatua kupitia vyama vya Michezo kuweza kujiendesha na kufanya shughuli zake za kawaida za kimechezo.
Aidha amesema suala hilo limekuja baada ya SMZ kutaka kila mwanamichezo kuweza kufaidika na kuweza kujiajiri kwenye sekta ya michezo ili kuweza kupambana na maisha ya kawaida na maendeleo ya michezo visiwani Zanzibar Khamis Mzee amengeza kusema vyama vya michezo vinamajukumu ya kuhakikisha wanapiga maendeleo.
Kwa upande mwengine amesema sera hiyo imeweza kufanyiwa marekibisho ili iweze kutekelezeka kwa vitendo ikiwemo kuhakikisha kila mtu anashiriki michezo kwa maslahi ya Taifa na maslahi yake binafsi ili kutanua wigo wa mkubwa kwa vyama vya michezo kuweza kutoa wachezaji wenye uwezo wa kushiriki mashindano mbali mbali ndani na nje ya Zanzibar na kuzalisha vipaji vya wanamichezo Zanzibar.
Amevitaka vyama vya michezo Zanzibar vyote 36 kuhakikisha vinaweza kujitegemea na kuwa na miradi yao yenyewe na vilabu vyao ili kupunguza wimbi la utegemezi wa BMTZ moja kwa moja baadhi ya wakati BMTZ inakubwa na changamoto ya fedha.
‘’Mwaka wa fedha Raisi Dk Ali Mohamed Shein ameahidi kuongeza fedha kwenye Wizara yetu ya Vijana Sanaa na michezo nategemea BMTZ tunaweza sana kusaidia vyama vya michezo mwaka huu ili kuweza kuendesha mashindano ya kimataifa ndani na nje ya Zanzibar na kuweza kusafirisha timu zetu zote za Taifa’’ Alimalizia Khamis Abdalla.
Bausi ateta ukimya wa Uchaguzi ZFA
Kufuatia ukimya mkubwa sakata la Uchaguzi ndani ya Chama cha mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) tangu kuundwa kamati ya muda na Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Walace Karia mwaka jana mwezi wa Tano hadi sasa.
Gazeti hili limezugumza na Mchezaji wa Zamani wa Black Fighter na timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi ambaye pia aliwahi kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar amesema kitendo cha kuendelea soka la Zanzibar kuongozwa na kamati ni kinyume na taratibu za mpira miguu duniani .
Aidha Bausi amesema kitendo cha kuwa kimya muda mrefu sana masuala ya uchaguzi na katiba ndani ya ZFA ni dalili za wazi kuwa masuala ya uchaguzi ndani ya ZFA yanaweza kuwa hayapo tena au kuchelewa kwa muda mrefu hivyo ameliomba BMTZ kuhakikisha inatimiza wajibu wake kusimamia uchaguzi wa ZFA.
Kwa upande mwengine Salum Bausi amesema kitendo cha mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar kuifuta kamati tendaji ya ZFA na wao ndio wapitishaji wa Katiba mpya ya ZFA kinatia wasi wasi mkutano mkuu upi utakao kwenda kupitisha katiba mpya na kupata vingozi wapya ndani ya ZFA.
‘’Mwaka 2014/2015 ambapo ZFA ilikuwa ikiongozwa na kamati ya Hussein Ahmada tulitaka kutolewa kwenye mashindano ya CECAFA yaliofanyika Ethopia lakini kwa huruma ya Nicholous Musonye na Ludinga Tenga tukaachiwa kwa sababu sisi ni wanzilishi wa Goseji CECAFA tujifunze kupitia ya nyuma ‘’ Alifafanua Salum Bausi.
Salum Bausi ambaye pia aliwahi kuwa mgombea wa Uraisi wa ZFA mwaka 2013 amesema mchakato wa katiba ndani ya ZFA hauweza kuchukua muda mrefu lakini kwa ZFA mpaka sasa mchakato huo umekuwa na kimya muda mrefu na kusema kwa sasa ZFA inahitaji kuwa na Viongozi bora watakao weza kulisaidia soka la Zanzibar.
‘’Tuliambiwa uchaguzi utafanyika baada ya michuano ya Kombe la Mapinduzi lakini tunaonana kimya sana sasa huko baadae mbele hatujui haya mambo yatakuwa vipi mpira wetu umekuwa mgumu sana tunahitaji kurejesha haiba ya mpira wetu wa zanzibar’’ Alimalizia Salum Bausi.
Monday, January 21, 2019
ZAHA kufanya tathimni ya mpira wa mikono
Chama cha mpira wa mikono Zanzibar (ZAHA) kimefanya tasmini ya mashindano ya Mapinduzi Cup yaliomalizika Kisiwani Pemba baada ya kilele cha Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizugumza na Gazeti hili mratibu wa mafunzo ndani ya chama hicho Kombo Ali amesema kwa muda mrefu ZAHA imekuwa ikiendesha mashindano na mafunzo ndani ya kisiwa cha Unguja na Pemba kukosa fursa za maendeleo ya mchezo huo.
Aidha amesema baada ya kumalizika mashindano ya mpira wa mikono mapinduzi Cup kisiwani Pemba ni wazi kwa sasa mchezo huo unakwenda kubadilika na kukabalika kisiwani Pemba na kuwa na vilabu vingi vya Ligi kuu ya Mpira wa mikono Zanzibar badala ya kutegemea vikosi vya SMZ.
Aidha amesema mafunzo maalum yamesaidia kuwajenga uwalewa kwa Vijana uwelewa wa mchezo huo kwa ngazi ya awali na kuhakikisha mchezo huo unazalisha wachezaji wengi kama ulivyo mpira wa miguu Visiwani Zanzibar.
‘’Tukitaka tupige hatua kwanza tuwe na vilabu vingi tuwe na mashindano mengi ili hamasa ingie sana sisi ni moja ya chama ambacho tunamalengo ya kukuza mchezo huo Tanzania kwa ujumla ‘’ Alisema Kombo Ali.
Kwa upande mwengine amesema wanatarajia kuwa na mashindano ya Vijana ya Wilaya ya kati kwa lengo kuusambaza mchezo huo maeneo yote Unguja na Pemba.
Subscribe to:
Posts (Atom)