Monday, January 21, 2019

ZAHA kufanya tathimni ya mpira wa mikono

Chama cha mpira wa mikono Zanzibar (ZAHA) kimefanya tasmini ya mashindano ya Mapinduzi Cup yaliomalizika Kisiwani Pemba baada ya kilele cha Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. Akizugumza na Gazeti hili mratibu wa mafunzo ndani ya chama hicho Kombo Ali amesema kwa muda mrefu ZAHA imekuwa ikiendesha mashindano na mafunzo ndani ya kisiwa cha Unguja na Pemba kukosa fursa za maendeleo ya mchezo huo. Aidha amesema baada ya kumalizika mashindano ya mpira wa mikono mapinduzi Cup kisiwani Pemba ni wazi kwa sasa mchezo huo unakwenda kubadilika na kukabalika kisiwani Pemba na kuwa na vilabu vingi vya Ligi kuu ya Mpira wa mikono Zanzibar badala ya kutegemea vikosi vya SMZ. Aidha amesema mafunzo maalum yamesaidia kuwajenga uwalewa kwa Vijana uwelewa wa mchezo huo kwa ngazi ya awali na kuhakikisha mchezo huo unazalisha wachezaji wengi kama ulivyo mpira wa miguu Visiwani Zanzibar. ‘’Tukitaka tupige hatua kwanza tuwe na vilabu vingi tuwe na mashindano mengi ili hamasa ingie sana sisi ni moja ya chama ambacho tunamalengo ya kukuza mchezo huo Tanzania kwa ujumla ‘’ Alisema Kombo Ali. Kwa upande mwengine amesema wanatarajia kuwa na mashindano ya Vijana ya Wilaya ya kati kwa lengo kuusambaza mchezo huo maeneo yote Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment