Wednesday, January 30, 2019

Stika ataka sera ya ya filamu itekelezwe

Chama cha wasanii Filamu Zanzibar wameiomba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuharikisha kupitishwa sera yao ya Filamu na maigizo ya mwaka 2015. Akizugumza na Gazeti hili Katibu wa chama cha Filamu Zanzibar Salum Maulid Salum (Stika) amesema kwa muda mrefu baada ya kupitisha sera hiyo mwaka 2015 ya rasimu ya pili mpaka leo sera hiyo bado haijafanyiwa kazi na kufanya chama chao kutokuwa na sera ya kufanya kazi zao kitaalam. Aidha Salum Stika amesema sera hiyo itapopitishwa kwenye Baraza la Wakilishi na kupatiwa michango chama chao kitakuwa na jitihada ya kuhakikisha filamu za maigizo Zanzibar zinakwenda kufanyiwa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji na kuendeshwa katika viwango vikubwa. Kuhusu Soko la Filamu Zanzibar amesema wasanii wengi Zanzibar wanalalamikia mfumo wa soko Zanzibar lakini amesema changamoto hiyo itandoka baada ya sera ya mwaka 2015 kufanyiwa marekibisho na Baraza la wakilishi. ‘’Tunamuomba sana Wazara ya Vijana Sanaa na Michezo ihakikishe mwaka huu sera yetu ya sanaa ya Filamu na Maigizo inapelekwa kwenye Baraza la wakilishi na kufanyiwa marekibisho ili kuwa katika viwango vya ubora’’ Alilimalizia Salum Stika.

No comments:

Post a Comment