Friday, January 25, 2019

Bausi ateta ukimya wa Uchaguzi ZFA

Kufuatia ukimya mkubwa sakata la Uchaguzi ndani ya Chama cha mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) tangu kuundwa kamati ya muda na Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Walace Karia mwaka jana mwezi wa Tano hadi sasa. Gazeti hili limezugumza na Mchezaji wa Zamani wa Black Fighter na timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi ambaye pia aliwahi kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar amesema kitendo cha kuendelea soka la Zanzibar kuongozwa na kamati ni kinyume na taratibu za mpira miguu duniani . Aidha Bausi amesema kitendo cha kuwa kimya muda mrefu sana masuala ya uchaguzi na katiba ndani ya ZFA ni dalili za wazi kuwa masuala ya uchaguzi ndani ya ZFA yanaweza kuwa hayapo tena au kuchelewa kwa muda mrefu hivyo ameliomba BMTZ kuhakikisha inatimiza wajibu wake kusimamia uchaguzi wa ZFA. Kwa upande mwengine Salum Bausi amesema kitendo cha mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar kuifuta kamati tendaji ya ZFA na wao ndio wapitishaji wa Katiba mpya ya ZFA kinatia wasi wasi mkutano mkuu upi utakao kwenda kupitisha katiba mpya na kupata vingozi wapya ndani ya ZFA. ‘’Mwaka 2014/2015 ambapo ZFA ilikuwa ikiongozwa na kamati ya Hussein Ahmada tulitaka kutolewa kwenye mashindano ya CECAFA yaliofanyika Ethopia lakini kwa huruma ya Nicholous Musonye na Ludinga Tenga tukaachiwa kwa sababu sisi ni wanzilishi wa Goseji CECAFA tujifunze kupitia ya nyuma ‘’ Alifafanua Salum Bausi. Salum Bausi ambaye pia aliwahi kuwa mgombea wa Uraisi wa ZFA mwaka 2013 amesema mchakato wa katiba ndani ya ZFA hauweza kuchukua muda mrefu lakini kwa ZFA mpaka sasa mchakato huo umekuwa na kimya muda mrefu na kusema kwa sasa ZFA inahitaji kuwa na Viongozi bora watakao weza kulisaidia soka la Zanzibar. ‘’Tuliambiwa uchaguzi utafanyika baada ya michuano ya Kombe la Mapinduzi lakini tunaonana kimya sana sasa huko baadae mbele hatujui haya mambo yatakuwa vipi mpira wetu umekuwa mgumu sana tunahitaji kurejesha haiba ya mpira wetu wa zanzibar’’ Alimalizia Salum Bausi.

No comments:

Post a Comment