Wednesday, January 30, 2019
ZFA kuja na mipango kazi
Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetangaza kuwa na mpango kazi wake wa maendeleo kuanzia mwaka 2019 hadi 2022 kwa ngazi zote zinazo husu mpira Zanzibar.
Akizigumza na wandishi wa habari mkuregenzi wa ufundi wa ZFA Salum Ali Haji amesema ZFA baada ya muda mrefu kushindwa kufanya mipango yake ya uhakika sasa kamati imeamua kuja na mipango ya maendeleo ya soka ndani ya visiwa vya Zanzibar wakianza na elimu ya mpira kwa wadau ili kujua maana ya mchezo huo unaopendwa lakini wamekosa ufahamu wa mchezo huo.
Aidha amesema kwa mwaka huu 2019 wamejipanga kuhakikisha Vijana wengi maskulini wanashiriki mchezo wa mpira wa miguu kutokana na umri wao na madaraja yanavyotakiwa ili kuweza kutoa wachezaji wengi maskulini wenye uwezo wa kucheza mpira kwenye viwango vya kimataifa.
Kwa upande mwengine amesema mwaka 2019/2020 ZFA itakuwa na mikakati ya maendeleo ya kukuza soka kwa kutoa mafunzo kwa makocha wote wasio na leseni hata moja na wale wenye leseni ndogo kupatiwa mafunzo ya juu ya ukufunzi ili kwa mwaka huo Zanzibar kuwe na wakufuzi wenye leseni kubwa, Salum amesema mafunzo mengine ni ya Udaktari wa viungo na michezo na semina za uongozi wa mpira kwa viongozi wote kunzia Wilayani hadi ZFA Taifa.
‘’Tumekaa na Wizara ya Elimu kupitia idara ya Elimu na Michezo tumehakikisha tunafanya mashindano ya Vijana ya maskulini ya Wilaya na kundaa Vijana kuwa wakufunzi na waamuzi wa baadae jambo hili lilikuwepo ila sasa ZFA tunakwenda kulifufua’’ Alisema Salum Haji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment