Friday, January 25, 2019

BMTZ vyama vinaweza kujiendesha zanzibar

Baraza la Michezo Zanzibar (BMTZ) limejipanga kuhakikisha vyama vya michezo Zanzibar vinaweza kujiendesha bila ya kutegemea ruzuku ya Baraza la Michezo inayotolewa kwa kila chama cha Michezo . Akizugumza na Mtandao huu
Katibu Mtendaji wa BMTZ Zanzibar Khamis Abdalla Mzee amesema kwa mwaka 2019 BMTZ imefanyia marekibisho sera ya michezo Zanzibar ili kuona sekta ya michezo Zanzibar inapiga hatua kupitia vyama vya Michezo kuweza kujiendesha na kufanya shughuli zake za kawaida za kimechezo. Aidha amesema suala hilo limekuja baada ya SMZ kutaka kila mwanamichezo kuweza kufaidika na kuweza kujiajiri kwenye sekta ya michezo ili kuweza kupambana na maisha ya kawaida na maendeleo ya michezo visiwani Zanzibar Khamis Mzee amengeza kusema vyama vya michezo vinamajukumu ya kuhakikisha wanapiga maendeleo. Kwa upande mwengine amesema sera hiyo imeweza kufanyiwa marekibisho ili iweze kutekelezeka kwa vitendo ikiwemo kuhakikisha kila mtu anashiriki michezo kwa maslahi ya Taifa na maslahi yake binafsi ili kutanua wigo wa mkubwa kwa vyama vya michezo kuweza kutoa wachezaji wenye uwezo wa kushiriki mashindano mbali mbali ndani na nje ya Zanzibar na kuzalisha vipaji vya wanamichezo Zanzibar. Amevitaka vyama vya michezo Zanzibar vyote 36 kuhakikisha vinaweza kujitegemea na kuwa na miradi yao yenyewe na vilabu vyao ili kupunguza wimbi la utegemezi wa BMTZ moja kwa moja baadhi ya wakati BMTZ inakubwa na changamoto ya fedha. ‘’Mwaka wa fedha Raisi Dk Ali Mohamed Shein ameahidi kuongeza fedha kwenye Wizara yetu ya Vijana Sanaa na michezo nategemea BMTZ tunaweza sana kusaidia vyama vya michezo mwaka huu ili kuweza kuendesha mashindano ya kimataifa ndani na nje ya Zanzibar na kuweza kusafirisha timu zetu zote za Taifa’’ Alimalizia Khamis Abdalla.

No comments:

Post a Comment