Wednesday, January 16, 2019

Anguko la Soka Kisiwani Pemba latajwa

Wadau wa soka kisiwani Pemba wamefunguka sababu ya kuanguka soka ndani ya kisiwa hicho ni ongezeko la gharama za kuendesha timu kulingana na mahitaji ya sasa. Wakizugumza na Gazeti hili wadau mbali mbali wa mpira wa miguu Kisiwani Pemba Ali Hamad mkaazi wa Wete amesema sababu ya kunguka soka kisiwani Pemba ni kutokana na mindombinu mibovu ya kuendeshea soka kwa Zanzibar nzima. Aidha Hamadi amesema kitendo cha ligi kuu ya Zanzibar kuchezwa kwa misimu 6 bila ya mdhamini ni sawa na kucheza ngoma ambayo huijui hivyo muda umefika kwa wahusika waliobeba dhamana kushindwa kutumiza wajibu wao. Said mrisho mkaazi wa machomane eneo la kambi ya timu ya Chupkizi amesema kitendo cha vilabu vya Pemba kufanya vibaya kwenye Ligi kuu ya Zanzibar msimu huu ni dalili ya wazi kuwa soka la kisiwani Pemba liko chini na linahitaji uwekezaji mkubwa sana ili kundoa changamoto ndani ya vilabu vya Pemba. ‘’Siasa yetu imechangia sana kuharibu soka letu la Zanzibar kwa Unguja na Pemba tumegawanywa sana sisi Pemba tunaonekana tuko nyuma leo Pemba kunaonekana mbali sana wakati sisi ni wamoja lazima turudi kwenye umoja ndio uhai wa soka letu la Zanzibar’’ Alifafanua Mrisho. Kwa upande wake baadhi ya Vijana wanaocheza ligi za madaraja ya Vijana kisiwani Pemba wamesema kitendo cha ZFA kutokuwa na ufatiliaji wa kutafuta vipaji kutoka Pande ya Pemba na kubedhi Unguja kinaleta mgawanyo na hakijengi umoja kwenye soka la Zanzibar.

No comments:

Post a Comment