Tuesday, January 15, 2019

SMZ kuongeza bajeti ya michezo mwaka wa fedha

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema iko katika mpango wa kuongeza bajeti ya Wizara ya michezo kwenye mwaka ujao wa fedha ili kuvisaidia vyama vya michezo Zanzibar na kundeleza michezo Zanzibar. Akizugumza kwenye shamrashamra za kusherekea miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar Kisiwani Pemba Afisa mdhamini michezo na utamaduni Shein Ali amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa makusudi imeamua kundeleza suala la michezo yote Zanzibar ikiwemo michezo ambayo inachezwa hadharani bila va vingilio ili kuweza kuwasaidia wanamichezo. Aidha amesema sekta ya michezo bado inakubwa na changamoto ya fedha ila bado anawapongeza Vijana kujitoa kuhakikisha wanafanya bidii ya kuweza kujiajiri kwenye sekta ya michezo Zanzibar. ‘’Kwenye ilani ya CCM 2015 -2020 imeeleza wazi suala la michezo ni ajira hivyo kwa makusudi tumeamua kulipa suala hili kipao mbele ikiwemo ujenzi wa Viwanja vya kisasa kwenye kila wilaya za Unguja na Pemba na ujenzi wa kiwanja cha Mao Zendog yote ni mafanikio yetu’’ Alisema Ali Shein.

No comments:

Post a Comment