Wednesday, January 16, 2019

Pemba wataka Mchezo wa Ng'ombe uboreshwe

Wananchi wa kisiwani Pemba na wakaazi wa Kiuyu Nungwini wameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Sanaa Vijana na Michezo kuendeleza michezo ya asili ili kulinda utamaduni wa mzanzibar. Akizugumza na mtandao huu mchezaji mkongwe wa mchezo wa Ng’ombe Abdalla Ali wakati wa shamra shamra za kuelekea kilele cha mapinduzi ya Zanzibar ya miaka 55 huko Kiuyu Pemba amesema mchezo huo kwa sasa unaelekea kufa baada ya wachezaji wengi wa mchezo huo kuwa ni watu wazima na umri wao umeshakwenda . Aidha ameitaka Serikali ya SMZ kuhakikisha inaendeleza mchezo huo kwa Vijana kwa kujengewa uwanja maalum wa kisasa wa mchezo huo kama unavyofanywa kwenye nchi zilizoendelea ili kutengeneza usalama kwa wanaongalia mchezo huo na wachezaji badala yake kuachana na dhana ya kuchezwa kwa wakati maalum. Kwa upande wake mchezaji mkongwe wa mchezo huo Ali Azan amesema mchezo huo umekuwa uko hatarini kupotea kutokana na Vijana kuwa woga wa kucheza na Ng’ombe badala yake Vijana wamefata michezo ya kisasa na kuacha ya asili. ‘’Sisi tunacheza mchezo huu miaka 50 sasa tushavunjwa sana na Ng’ombe lakini tunauguza miguu baadaye tunaendelea na mchezo huu kama vile mpira wa miguu unapata majeraha unarudi uwanjani’’ Alimalazia Azani Ali. Kwa upande Makamo pili wa Raisi Zanzibar Balozi Sefu Ali Idi amewakabidhi wachezaji TSH laki tano na kuahidi Serikali ya SMZ itandeleza mchezo huo kwa upande wa kisiwa cha Pemba.

No comments:

Post a Comment