Tuesday, January 15, 2019

Mashindano ya mpira wa mikono Mapinduzi Cup 2019 yamehitimishwa rasmi kisiwani Pemba baada ya kupatikana washindi wa nne wa mchezo huo. Akizugumza wakati akifunga mashindano hayo Naibu waziri nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na Idara maalum (SMZ) pia ni mwakilishi wa micheweni Shamata Khamis amesema jitihada za makusudi zinahitajika ili kukuza mchezo huo kuanzia ngazi za watoto ili kuwa na wachezaji wengi kwenye mchezo huo. Aidha ameiomba Serikali ya SMZ Kuhakikisha wanaweka kipao mbele michezo midogo midogo ambayo ina sifa ya kutawakilisha vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na kuitangaza nchi yetu kwenye Nyanja zote. ‘’Mchezo huu umekuja kuleta changamoto hapa kisiwani Pemba upo chini sana tofauti na mpira wa miguu sasa tunakwenda kuanza mchezo huu rasmi kisiwani Pemba’’ Alisema Shamata. Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo pia ni mjumbe wa ZAHA Kombo Ali amesema mashindano hayo yamefanyika yakiwa na changamoto kubwa ya udhamini na kusababisha changamoto kubwa. ‘’Mchezo huu ni wa wazi hauna vingilio kwa hapa kwetu sasa tunaiomba sana Serikali na wadau wengine wa mpira wa mikono inatuunga mkono’’ Alimalizia Kombo Ali. Mashindano ya Mpira wa mikono Mapinduzi Cup 2019 yamemalizika kwa kundaliwa mafunzo maalum kwa wachezaji wapya wa mpira wa mikono na Klabu ya Ngome kutoka Tanzania bara wanaume wamefanikiwa kuwa mabingwa,na kwa wanawake Ngome pia wamefanikiwa kuwa mabingwa, mshindi wa kwanza Vijana Data kutoka Tanga na kwa wanawake Vijana klabu ya Uzini. ............................................................................................. 3 Attachments

No comments:

Post a Comment