Wednesday, January 16, 2019

Neema ya washukia michezo ya walemavu zanzibar

Chama cha mpira wa miguu wa walemavu wa Zanzibar wanatarajia kupata udhamini kutoka chama cha mpira wa walemavu duniani kuanzia mwezi ujao wa pili. Akizugumza na Gazeti hili mwenyekiti chama hicho hapa visiwani Zanzibar Hassan Haji Silima amesema chama cha mpira wa miguu watu wenye ulemavu Zanzibar wanatarajia kupokea msaada wa udhamini wa vifaa vya kisasa ili kuweza kushiriki mashindano ya kimataifa bila ya kuwa na changamoto ya vifaa vya mchezo huo. Aidha Silima amesema baada ya ziara ya Raisi wa Shirikisho la mpira wa miguu watu wenye ulemavu Dunia Zanzibar Samuel Backer mwaka uliopita amewaahidi kuwaletea vifaa vya kisasa ili kuweza kuwasaidia watu wenye ulemavu Zanzibar kuweza kushiriki kwenye michezo ya kimataifa. Kuhusu Ligi kuu ya Zanzibar ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu amesema kwa muda mrefu sana mashindano hayo yamekuwa yakisita kutokana na kukosa vifaa vya kisasa na kusababisha Ligi hiyo kuzorota na idadi ndogo ya vilabu vya watu wenye ulemavu Zanzibar . ‘’Ukweli hamasa bado ndogo ila tunatarajia baada ya kupata vifaa hivi hamasa itaongezeka kwa wachezaji wetu maana watu wenye ulemavu bado wanajiona wao ni wanyonge sana’’ Alimalizia Silima.

No comments:

Post a Comment