Wednesday, January 16, 2019

JKU yapania Ubingwa Ligi Kuu Zanzibar ZPL.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar JKU wanaendelea na kujipanga kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Zanzibar baada ya kumaliza mzunguko wa mwanzo wa Ligi kuu ya Zanzibar (ZPL) huko kisiwani Pemba wakiwa nafasi ya 4 alama 38. Akizugumza na Gazeti hili msemaji wa klabu hiyo Said Salim amesema wao Jku baada ya kutolewa kwenye hatua ya awali ya mashindano ya Vilabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Al Hilal hawakuwa na budi tena kuelekeza silaha kwenye Ligi kuu ya Zanzibar msimu huu ili kuweza kutetea taji lao. Aidha Salim amesema walikuwa na viporo vingi vilivyofanya klabu yao kuwa na ratiba ngumu ya Ligi hivyo waliweza kupambana na kufika hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar. Kwa upande mwengine Salim amesema sasa klabu yao watakwenda mapunzikoni kwa muda ila baada ya hapo timu itaendelea na mazoezi ili kujipanga kuleta ushindani na kutetea taji lake la Ligi kuu ya Zanzibar msimu huu. ‘’Tunashukuru tumemaliza mzunguko wa mwanzo tukiwa tumeshinda michezo 10 mfulilizo bila ya kufungwa hata mmoja huku kisiwani Pemba ni dalili ya kuwa sisi ni Mabingwa tena msimu huu hili halina mjadala’’ Alisema Salim Said. Ligi kuu ya Zanzibar imemaliza mzunguko wa mwanzo Kvz wapo kileleni wakiwa na alama 41, Kmkm nafasi ya pili wakiwa na alama 37 sawa na Jku na Mafuzo tofauti ya magoli tu.

No comments:

Post a Comment