Wednesday, January 16, 2019
ZFA yatakiwa kulelea vipaji
Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetakiwa kundelea kukuza vipaji vya wachezaji Vijana ili kuwa na wachezaji wengi kwenye timu za Taifa za Tanzania na zile za Zanzibar ili kuendeleza soka la Tanzania kwa ujumla.
Akizugumza na mtandao huu Mkuregenzi wa ufundi wa TFF Amy Ninje akiwa Zanzibar kwenye zoezi la utafutaji vipaji vya timu ya Taifa ya Tanzania U 17 ya baadae amesema Zanzibar ni moja ya visiwa vilivyojaaliwa kuwa na vipaji ambavyo vinaweza kuuzika sehemu mbali mbali duniani.
Amesema ZFA wanahitaji kuwa na mipango ya muda mrefu kukuza soka la Vijana kwa kuwa Vijana wa Zanzibar wanakulia kwenye damu ya mpira ila wanahitaji kuendelezwa ili kuhakikisha wanapiga hatua kama Zanzibar kuwa na wachezaji wazuri ili kuwakilisha pande zote mbili kwenye timu za Taifa.
Aidha kuhusu Zoezi la kutafuta vipaji amewapongeza ZFA kwa kundaa Vijana wengi kwenye hatua hiyo ya kutafuta vipaji ambayo ni moja ya ajenda ya TFF kukuza soka la Vijana ili kuwa na timu bora za baadae .
Kwa upande mwengine amesikitishwa na kitendo cha Zanzibar kushindwa kupeleka timu ya Taifa ya U20 kwenye mashindano ya CECAFA Uganda kwa vile Zanzibar kuna timu wachezaji na timu nyingi za Vijana ambazo zingeweza kuifanya Zanzibar kuonyesha uwezo wao wa kucheza soka.
‘’ katika mipango yangu nimekaa na ZFA kuna mashindano ya Vijana tuyanzushe Taifa Cup ili kuwa na mashindano ya kanda ya Vijana ya ndani ya Tanzania ‘’Alisema Amy Ninje.
Jumla ya wachezaji 13 wamechaguliwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya Taifa ya Tanzania wataelekea Arusha kwenye kambi maalum ya pamoja kuungana na wenzao wa mikoa mengine ya Tanzania bara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment