Saturday, January 19, 2019
Kusini walalamika ubovu wa soka la vijana
Chama cha mpira wa miguu ZFA wilaya ya kusini Unguja kimesikitishwa na uendashaji mbovu wa soka la Vijana ndani ya Wilaya yao na kufanya timu zao kutofanya vizuri kwenye mashindano mbali mbali kwa muda mrefu.
Akizugumza na Gazeti hili Katibu Mkuu wa ZFA Wilaya ya Kusini Unguja Aje Usi Mbwana amesema kitendo cha timu ya kombaini ya Wilaya ya Kusini ya Vijana kufanya vibaya kwenye mashindano ya Vijana yaliondaliwa na ZBC Mapinduzi Cup na kufugwa magoli mengi michezo yote ni dalilia ya wazi uendashwaji mbovu wa soka la Vijana Kusini Unguja .
Aidha Usi ameelezea changamoto ya soka la Vijana ndani ya Wilaya yao tofauti na Wilaya nyengine za Zanzibar kutokana mifumo ya ungozi waliobeba dhamana ya kuongoza soka la Vijana ndani ya Wilaya ya kusini Unguja wameshindwa kusimamia kanuni za mpira badala yake wamekimbilia kwenye maslahi yao binafsi na kupelekea soka la Vijana Kusini Unguja kuwa kwenye kiwango cha chini sana.
Kwa upande wa vilabu amesema licha ya jitihada kubwa zinaoyeshwa na vilabu ndani ya Wilaya yake hususan za madaraja ya Vijana na kuwa na vilabu vichache kwenye Wilaya ya Kusini Unguja ndio sababu nyengine ya kuanguka soka la Vijana.
‘’Unapo kuja uchaguzi hapa viongozi wote hukimbilia mjini kwenye ujumbe wa ZFA Taifa sisi tunachiwa mzigo mzito wa kundesha soka la Vijana na wakubwa ndani ya Wilaya yetu bado hatuna viongozi wenye nia ya kuongoza soka la Vijana ndani ya Wilaya yetu ‘’ Alimalizia Usi Mbwana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment