Wednesday, January 16, 2019

RC Ayubu awapongeza wilaya mjini ZBC Mapinduzi Cup

Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharib Ayubu Mohamed Mahumud amewaahidi zawadi washindi wa mashindano ya Ligi za madaraja ya Vijana Wilaya ya Mjini na Magharib msimu huu wa mwaka 2018/2019. Akizugumza kwenye mapokezi ya timu ya Vijana ya wilaya Mjini hapa visiwani Zanzibar baada ya kuibuka mabingwa mara ya pili kwenye mashindano ya ZBC watoto Mapinduzi Cup yaliomalizikia kisiwani Pemba na Wilaya ya Mjini kuwa mabingwa. Aidha Ayubu amewataka Vijana hao kundelea kudumisha nidhamu ya michezo ili kuweza kuleta maendeleo ya michezo visiwani Zanzibar na kuwa wachezaji tegemezi baadae kwenye vilabu vikubwa ndani na nje ya Tanzania. ‘’Vingozi wenu ni imara kila jambo wanalolindaa vizuri na mapema walikuja ofisini kwangu tunapanga kwa pamoja sasa mwaka huu nimeahidi kusaidia wilaya hizi mbili ili kutoa hamasa kwa vijana’’ Alifafanua Ayubu. Kwa upande wake Katibu wa kamati ya soka la Vijana Wilaya ya mjini Alawi Haidar amesema wilaya ya mjini ni wilaya kubwa kimechezo hususan mpira wa miguu ndio wilaya iliyozalisha wachezaji wengi wenye majina kutoka madaraja ya Vijana . ‘’Feisal Salum, Nadir Haroub, Saidi Makapu, Angrey Morris, Sleman Selembe na wachezaji wote wa Zanzibar Heros chimbu lake ni Wilaya ya mjini ‘’ Alimalizia Alawi Foum. Mkuu wa mkoa mjini Magharib amewaihidi mabingwa wa ngazi zote za Ligi za Vijana Wilaya ya mjini na Magharib viatu ,seti za jezi fedha taslim na vifaa maalum kundeshea ofisi za wilaya hizo za ZFA za madaraja ya Vijana. Wilaya ya mjini imefanikiwa kuchukua kombe hilo la ZBC watoto Mapinduzi Cup baada ya kuifunga wilaya ya Magharib B magoli 2 kwa moja kwenye uwanja wa Gombani.

No comments:

Post a Comment