Monday, January 21, 2019

BMTZ kuendeleza michezo Zanzibar

Baraza la Michezo la Taifa Zanzibar (BMTZ) limesema halitovifutia usajili vyama vya michezo ambavyo vinashindwa kuendesha mashindano yake ya ndani na kufanya shughuli zake za kawaida sababu baraza hilo lipo kwa jiili ya kuinua michezo si kudumaza michezo Visiwani Zanzibar. Akizugumza na mtandao huu
kwenye mahujiano maalum huko Ofisi ya BMTZ Mwanakwerekwe Katibu Mtendaji wa BMTZ Khamis Abdalla Mzee amesema BMTZ ina lengo la kulea michezo visiwani Zanzibar hivyo vyama vya michezo haviwezi kufutwa kwa sababu ya kutoshindwa kuendesha mashindano baraza hilo linatambua umuhimu wa vyama vya michezo Zanzibar. Aidha amesema BMTZ imesajili jumla ya vyama 36 vya michezo ila vyama 24 ndio vinavyofanya vizuri na kufanya shughuli zake kwa kufuata kalenda zao walizojiwekea na kulipa ada ndani ya Baraza la Michezo na kuwa karibu na BMTZ kwa mwaka 2018. Khamis Abdalla amesema BMTZ inajua changamoto zinazoikumba vyama vya michezo Zanzibar ikiwemo ukosefu wa vifaa na viwanja vya kuchezea baadhi ya michezo ila wao BMTZ iko bega kwa began a vyama vyote vya michezo ili kupata muwafaka wa changamoto zinazoikumba vyama vya michezo. Kwa mwaka 2018 Khamis Abdalla amesema vyama vitano tu vya michezo ambavyo vimefanya vizuri kwenye utandaji wa shughuli zao za michezo Kitaifa na Kimataifa ni Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA), Chama cha riadha Zanzibar (ZAAA) Chama cha mpira wa mikono Zanzibar (ZAHA) ,Chama cha mchezo wa karate na judo,Taekwondo, Chama cha mchezo wa kikapu (BAZA) . Kuhusu vyama 12 ambavyo havikufanya vizuri kwenye mwaka 2018 kuendesha shughuli zake zimetokana sababu mbali mbali ikiwemo ya ukosefu wa viwanja vya kisasa kama vile mchezo wa mpira wa magongo, Tennis, bao,Karata, chees ,kurusha mkuki na Gofu BMTZ ipo kutatua changamoto ya vyama hivyo. ‘’Mwaka 2019 sisi BMTZ malengo yetu ni kuhakikisha sera ya michezo inafanyiwa kazi baada ya kuhakikisha vyama vya michezo vyote vinaweza kujiendesha bila ya kutegemea ruzuku ya Baraza la michezo’’ Alimalizia Khamis Mzee.

No comments:

Post a Comment