Monday, January 21, 2019
ZTTA kuendesha mafunzo mwezi machi
Chama cha mpira wa meza Zanzibar (ZTTA) kimepongeza hatua ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga viwanja vya kisasa Mao Zedong ili kutanua sekta ya michezo Zanzibar.
Akizugumza na Gazeti hili Mjumbe wa kamati ya mpira wa meza Abubakar Khatib amesema hatua hiyo imekuja kubadilisha michezo Zanzibar na kuweka mazingira mazuri kwa wanamichezo visiwani Zanzibar ya kujitolea kwenye sekta ya michezo na kuzalisha ajira za michezo Zanzibar.
Kwa upande mwengine Kisandu amesema kitendo cha kujengewa ukumbi maalum kwa jiili ya mchezo wa mpira wa Meza Zanzibar inaweza kuinua chachu ya mchezo huo ambao zamani Zanzibar ilikuwa mabingwa wa mchezo huo Duniani na Afrika kwa ujumla ila ulipotea baada ya kutokuwepo viwanja vya kuchezea mchezo huo.
Aidha amesema baada ya kukabidhiwa ukumbi huo unaweza kutumia kwa mashindano ya wadogo na wakubwa ya Ligi kuu ya Zanzibar ili kuweza kushajihisha mchezo huo na kuona maeneo ya Zamani kufanyiwa marekebisho ya kisasa.
Kwa upande wa shughuli za chama hicho kwa mwaka 2019 amesema wanatarajia kuwa na mafunzo maalum ya mchezo huo yatakayofanyika Kisiwani Pemba mwezi wa tatu kwa walimu wa skuli za Pemba kwa lengo la kueneza mchezo huo upande wa pili wa Pemba ili kuwa na Ligi bora baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment