Tuesday, January 15, 2019

FA CUP zanzibar kuanza Febuary 5

Chama cha mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kupitia kamati ya mashindano imetangaza tarehe ya kuanza mashindano ya Kombe la FA cup Zanzibar linalotarajiwa kuanza tarehe 5 mwezi Febuary litashirikisha timu 24 kutoka daraja la kwanza na timu zote za daraja la pili Taifa na timu zote za Ligi kuu ya Zanzibar na timu za wilaya za wakubwa. Kwenye taarifa iliotolewa na katibu wa kamati ya mashindano Alawi Haidar Foum imesema mashindano hayo mapya ya FA CUP ambayo yameingizwa kwenye kanuni ya ZFA mshindi wa mashindano hayo atawakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani badala ya Makamo Bingwa wa Ligi kuu ya Zanzibar. Aidha taarifa hiyo inasema mashindano hayo yataanza kwa hatua ya mtoano kwa kanda ya Unguja na Pemba ili kundoa gharama zisizo za msingi na mwisho kupata timu nne kutoka kila kanda kucheza nane bora kutafuta mashindi mmoja wa mashindano hayo. Kwa upande wa vigezo imesema mshindi wa mashindano hayo itazingatia vigezo vya leseni za CAF za vilabu mwenye sifa ya kuwakilisha kwenye mashindano hayo ya Afrika kwa vilabu ngazi ya Kombe la Washindi. Wakati huo huo dirisha dogo la usajili tayari limefunguliwa rasmi na kufungwa janaury 25 .

No comments:

Post a Comment