Saturday, January 19, 2019
Salula ndoto zake kucheza nje ya Zanzibar
Mlinda mlango namba moja wa klabu ya Malindi visiwani Zanzibar amesema yuko tayari kusajiliwa klabu yeyote nje ya Zanzibar kuanzia sasa ili kuweza kutumiza ndoto zake.
Akizugumza na Gazeti hili Ahmedi Sleman Salula ambaye pia ni mlinda mlango namba mbili wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heros amesema mpira kwake ni kazi kama kazi nyengine hivyo yuko tayari klabu yeyote nje ya Zanzibar inayomtaka kumsajili yeye yuko tayari na kungalia maslahi yake mazuri.
Aidha amesema fununu zinazoenea mitaani kuwa huenda akasajiliwa Klabu ya Yanga baada ya kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Hemedi Sleman Moroko kumtaja kama kipa bora kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yaliomalizika visiwani Zanzibar amesema bado suala hilo si la kweli ila ni fununu tu zinazoenezwa mitaani.
‘’Unajua Yanga imekuwa kama timu ya nyumbani Zanzibar wako wengi sana wachezaji waliozaliwa na tumecheza pamoja Ligi kuu ya Zanzibar na Zanzibar Heros Feisal ,Abdalla Shaibu basi ikitokea kusajiliwa Yanga ntakuwa nipo nyumbani sijenda mbali’’ Alifafanua Ahmed Sleman.
Kuhusu michuano ya kombe la Mapinduzi timu yake kutolewa nusu fainali na Simba Salula amesema alizuhunika sana baada ya kuona kwa muda mrefu amekuwa mzoefu wa kucheza mashindano ya Kombe la Mapinduzi na timu yake kutolewa hatua ya Nusu Fainali aidha amesema sababu ya timu yake ya Malindi kufungwa ni kukosa umakini wa wachezaji.
‘’kwa sasa tunajindaa na Ligi kuu ya Zanzibar mwezi ujao ili kuweza kusaidia timu yetu kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Zanzibar na kuwakilisha kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika’’ Alimalizia Ahemedi Salula.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment