Wednesday, January 16, 2019
ZFA kusini yaunga mkono mabadiliko ya katiba
Chama cha mpira wa Miguu ZFA wilaya ya kusini kimesema kinaunga mkono mabadiliko yanayofanywa na ZFA Taifa ikiwemo mchakato wa katiba mpya ya ZFA.
Akizugumza na Gazeti hili Katibu wa ZFA wilaya ya Kusini Unguja Aje Usi Mbwana amesema wao wilaya wameyapokea mabadiliko hayo ambayo yanaweza kusaidia kupiga hatua mpira wa Zanzibar kwa miaka ijayo na kuleta utawala bora kwenye ZFA.
Amesema suala la katiba ya ZFA jambo muhimu kufanyiwa marekibisho licha baadhi ya vipengele vinakwenda kuwandosha vingozi wa muda mrefu wa ZFA ila katiba hiyo inakuja kuleta umoja ndani ya ZFA na kundosha makundi yalikuwepo kwa muda mrefu.
Kwa upande wa mabadiliko ya uendeshaji mpira wa Zanzibar kwenye katiba mpya ya ZFA amesema ni mafanikio makubwa sana siku za baadae Zanzibar kuwa na shirikisho la mpira wa miguu badala ya sasa kuwa na Chama cha mpira wa miguu inaweza kutanua utawala mpira kwenye maeneo makubwa ya mpira wa Zanzibar.
‘’Katiba inasema Wilaya zitajitegemea zitakuwa na katiba zao sio mbaya ni jambo jema ila wajue wilaya sasa hazitangiliwa na ZFA Taifa kama ilivyosasa haya mabadiliko ni mazuri kwetu’’ Alimalizia Aje Usi Mbwana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment